1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yaiangusha Ireland Kombe la Dunia la Wanawake

31 Julai 2023

Timu ya soka ya wanawake ya Nigeria imeingia hatua ya mtoano wa michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake baada ya mchezo wake wa leo dhidi ya Ireland kumalizika kwa kila upande kushindwa kutikisa nyavu za mwingine.

https://p.dw.com/p/4UbdJ
FIFA Fußball Frauen-WM | Australien vs Nigeria | Asisat Oshoala
Picha: James Whitehead/SPP/IMAGO

Matokeo hayo yameiweka Nigeria kwenye nafasi ya pili ya Kundi B nyuma ya mwenyeji mwenza wa michuano hiyo, timu ya soka ya wanawake ya Australia. 

Hivi sasa, Nigeria watakuwa na miadi na timu itakayoongoza Kundi D ambayo yumkini itakuwa timu ya soka ya England.

Soma zaidi: Nigeria yatinga raundi ya mtoano Kombe la Dunia
Nigeria yaibabua Australia Kombe la Dunia

Hiyo itakuwa ni mara ya tatu kwa kikosi hicho kinachofahamika kwa jina la utani la "Tai Wakubwa" kufika hatua ya 16 bora kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake. 

Mafanikio hayo ya leo yamelitoa kimasomaso bara la Afrika ambalo wawakilishi wake wengine ambao ni timu za Afrika Kusini, Zambia na Moroko zina matumaini madogo ya kusonga mbele.