1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria: Watu 168 hawajulikani walipo baada ya shambulio

4 Aprili 2022

Shirika la Reli Nigeria, NRC limesema watu 168 hawajulikani waliko baada ya shambulizi la kwenye treni kutokea wiki iliyopita na kuwaua watu wanane na wengine kadhaa kujeruhiwa.

https://p.dw.com/p/49Qif
Nigeria | Zugabteil der ersten Klasse
Picha: Olukayode Jaiyeola/NurPhoto/picture alliance

Mkurugenzi Mkuu wa NRC, Fidet Okhiria amesema katika taarifa yake iliyotolewa jana usiku kuwa watu 168 hawajulikani walipo.

Hata hivyo, hajasema iwapo wote hao ni abiria au wengine ni wafanyakazi wa shirika hilo.

Machi 28, watu wanaoshukiwa kuwa majambazi waliivamia treni inayofanya safari zake kutoka Abuja kwenda Kaduna kaskazini magharibi mwa nchi na kisha kufyatua risasi kwenye treni hiyo ya usiku.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusuika na shambulizi hilo.

Baadhi ya ndugu za watu ambao hawajulikani walipo, wamesema majambazi hao wamewasiliana nao wakisema wanawashikilia wapendwa wao.

Okhiria amesema watu 186 wamefika salama nyumbani, huku familia za watu 22 pekee wakiwa wameripoti kupotelewa na ndugu zao.