1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria: Wanamgambo 14 wa Boko Haram wauawa

29 Novemba 2017

Wanajeshi wa Nigeria wamewaua wapiganaji 14 wa Boko Haram katika operesheni ya kuliangamiza kundi hilo

https://p.dw.com/p/2oS5C
Nigeria Kampf gegen Boko Haram | ARCHIV
Picha: picture alliance /AP Photo/L. Oyekanmi

Wapiganaji 14 wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa na wanajeshi katika operesheni ya kupambana na ugaidi iliyofanyika kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Msemaji wa jeshi la Nigeria, Sani Usman, amesema jana kuwa wanajeshi hao waliwaokoa watu 30, wakiwemo watoto 15 katika operesheni hiyo iliyofanyika kwenye vijiji kadhaa kwenye jimbo la Borno mwishoni mwa juma lililopita.

Operesheni hiyo inahusisha mataifa kadhaa ya Afrika Magharibi katika mapambano ya miaka minane dhidi ya Boko Haram. Wanamgambo hao ni tishio katika jamii za kaskazini mashariki mwa Nigeria na wameanzisha mashambulizi katika nchi jirani za Chad, Niger na Cameroon.

Tangu mwaka 2009 maelfu ya watu wameuawa na Boko haram katika ukanda huo na inakadiriwa kuwa watu milioni 2.5 wameyakimbia makaazi yao. Lengo la kundi hilo ni kuanzisha utawala wa Sharia.