1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Niger yasitisha ushirikiano na shirika la IOF

26 Desemba 2023

Niger imesitisha ushirikiano na shirika la kimataifa la nchi zinazozungumza kifaransa, (IOF).

https://p.dw.com/p/4aamH
Waandamanaji wanaounga mkono mapinduzi katika mji mkuu wa Niamey
Waandamanaji wakiwa na bango dhidi ya Ufaransa wakati wa maandamano ya siku ya uhuru huko Niamey.Picha: AFP

Watawala wa kijeshi wamesema uhusiano kati ya Niger na mkoloni wake wa zamani Ufaransa umezidi kuharibika.

Msemaji wa jeshi wa Niger ameituhumu Ufaransa kwa kulitumia shirika hilo lenye wanachama 88 kama chombo cha kusimamia maslahi yake.

IOF imesema ilwiki iliyopita ilisimamisha baadhi ya mipango yake kwa Niger kwa sababu ya mapinduzi, hata hivyo shirika hilo limesema litaendelea na programu zinazowanufaisha watu moja kwa moja, pamoja na wanaochangia harakati za kurejesha demokrasia.

Soma pia: Ufaransa yawaondoa wanajeshi wake wa mwisho Niger 

Katika taarifa nyengine jeshi la Niger limesema bado halijaamua ni kwa muda gani litaendelea kushikilia madaraka, na kwamba muda wa kipindi cha mpito utabainishwa baada ya mazungumzo ya kitaifa ingawa halikutoa taarifa ni lini mazungumzo hayo yangefanyika.