1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali, Niger kujiondowa kwenye makubaliano na Ufaransa

6 Desemba 2023

Viongozi wa kijeshi wa Mali na Niger wamesema watafutilia mbali makubaliano ya ushuru na Ufaransa ndani ya miezi mitatu ijayo.

https://p.dw.com/p/4ZpPT
Waziri wa Nchi kwenye serikali ya kijeshi ya Mali, Kanali Abdoulaye Maiga.
Waziri wa Nchi kwenye serikali ya kijeshi ya Mali, Kanali Abdoulaye Maiga.Picha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Hii ni hatua nyingine ya kusambaratisha uhusiano na mkoloni huyo wa zamani, huku mataifa hayo jirani yakiimarisha mahusiano yao.

Katika taarifa ya pamoja, mataifa hayo ya Afrika Magharibi yamesema bado kunashuhudiwa "hali ya uhasama wa Ufaransa" dhidi ya mataifa yao na kusisitiza kuwa mikataba hiyo haina usawa na inasababisha hasara kubwa ya mapato kwa Mali na Niger.

Soma zaidi: Balozi wa Ufaransa aondoka Niger

Haikuwa wazi mara moja ni zipi athari za kiutendaji kufuatia uamuzi huo.

Ufaransa imekuwa na makubaliano ya ushuru na mataifa hayo kwa miaka mingi ambayo yanahusisha kodi ya mapato, ushuru wa urithi na ule wa usajili.

Mikataba hiyo inalenga kukuza ushirikiano katika masuala ya kifedha.