1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NICOSIA:Cyprus za Uturuki na Ugiriki zakubalina kuyafufua mazungumzo ya amani

9 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG9N

Viongozi wanaopingana wa Cyprus ya Ugiriki na Cyprus ya Uturuki wamekubalaiana kuyafufua mazungumzo ya amani kwa visiwa hivyo viwili vilivyogawika.

Juhudi za kuyafufua mazungumzo hayo zimefanikiwa kutokana na mjumbe wa Umoja wa mataifa Ibrahim Gambari huko Nicosia.

Bwana Ibrahim amesema mazungumzo hayo yataanza kufikia mwishoni mwa mwezi huu.

Mazungumzo hayo juu ya mapatano yalivunjika miaka miwili iliyopita baada ya Cyprus ya Uturuki kuipinga kura ya maoni iliyokuwa inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliyolengwa kumaliza mgawanyiko kati ya visiwa hivyo.