1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoQatar

Ni Japan au Croatia kuingia robo fainali?

5 Desemba 2022

Mechi za hatua ya mtoano katika michuano ya kombe la dunia zinaendelea sasa ambapo Japan inachuana na Croatia katika mchezo utakaomua timu itayojiunga na nyingine 4 zilizotangulia kuingia robo fainali.

https://p.dw.com/p/4KUmA
FIFA Fußball WM 2022 in Katar | Kroatien - Kanada | Tor  0-1
Picha: Hannah Mckay/REUTERS

Mshindi wa mechi ya jioni hii ndiye atapambana kwenye robo fainali na timu itakayoibuka kidedea katika mpambano mwingine wa baadaye leo usiku utakaozikutanisha Korea Kusini na miamba ya soka ya Amerika ya Kusini, timu ya taifa ya Brazil.

Tayari Uholanzi, Argentina, Ufaransa na England zimetangulia hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi katika michezo yao iliyopigwa mwishoni mwa juma.

Matumaini ya bara la Afrika yamesalia kwa timu ya taifa ya Morocco inayoteremka dimbani kesho dhidi ya Uhispania baada ya wawakilishi wengine wa bara hilo timu ya Senegal kufungashwa virago na England jana Jumapili.