1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malengo ya kundi la vijana wa Kongo wanaojiita "Wazalendo"

Saleh Mwanamilongo13 Aprili 2023

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kikosi cha kikanda kilichotumwa kusimamia amani eneo la mashariki kimesema kimezuia kutokea mapigano mapya baada ya kuzima mpango wa kundi la vijana wakongamani wanaojiita wazalendo kuzishambulia ngome za waasi wa M23 huko Kibumba. Inaaminika iwapo shambulizi lingetokea, makubaliano ya kusitisha mapigano huenda yangevunjika.Nini hasa asili ya kundi hilo?

https://p.dw.com/p/4Q1HU