1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEWYORK. Umoja wa mataifa waunga mkono azimio jipya.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNS

Baraza la Umoja wa mataifa limeunga mkono azimio jipya kuhusu silaha za kinuklia na maswala ya kigaidi.

Litakapopitishwa rasmi, azimio hilo sasa serikali za mataifa zitalazimika kuwafanyia mashtaka au kuwarudisha katika nchi walizotenda uhalifu watuhumiwa waliokamatwa na silaha za kinuklia au majarida yanayohusu mambo ya kinuklia ili wafunguliwe mashtaka.

Mswada huo dhidi ya kupambana na ugaidi ni wa kumi na tatu kuwasilishwa katika baraza la umoja wa mataifa na wa kwanza tangu shambulizi la kigaidi la septemba 11 lilipotokea nchini marekani.

Azimio hilo linahitaji kura ya ndio kutoka kwa mataifa wanachama 22 ili lipitishwe rasmi kuwa sheria ya kimataifa.