1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New_york: Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan...

26 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFoz

ameutaja mwaka huu unaomalizika wa 2003 kua mwaka ulioshuhudia mashaka makubwa kaabisa katika historia ya miaka 58 ya umoja wa mataifa.Katika hotuba yake ya nasaha ya mwaka mpya,katibu mkuu Kofi Annan amewataka walimwengu wajishughulishe zaidi hivi sasa na matatizo mengine muhimu,ambayo anasema,yanaweza pia kuhatarisha amani ya dunia.Ameyataja malengo ya Millenium yaliyopangwa kufikiwa hadi ifikapo mwaka 2015.Malengo hayo ni pamoja na kupambana na umasikini,njaa na maradhi.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kofi Annan amesema ahadi zilizotolewa wakati wa mkutano wa Millenium zinabiodi zitekelezwe kivitendo.Amesema sehemu ndogo tuu ya fedha zinazotumiwa kwa silaha zingetosha kukamilisha malengo hayo.