1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

News York. Baraza la usalama la umoja wa mataifa larefusha muda wa jeshi lake kulinda amani nchini Ivory Coast.

25 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF0F

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limerefusha muda wa jeshi lake la kulinda amani nchini Ivory Coast hadi Januari mwakani na kuamua kutuma wanajeshi 850 zaidi pamoja na polisi 375 wa kuimarisha kazi ya kulinda amani.

Ghasia zinazotokea chini kwa chini na kukaribia kulipuka zimeendelea kutokea nchini Ivory Coast, hasa jimbo lake la magharibi , kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi wa Oktoba.

Mazungumzo mapya ya kuleta amani yanayosimamiwa na Afrika kusini yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Pretoria kati ya rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na waasi.

Waasi wamekamata eneo la kaskazini la taifa hilo la Afrika magharibi katika mwaka 2002 baada ya jaribio lililoshindwa la kuipindua serikali.

Waasi na wanajeshi wanaomuunga mkono rais Gbagbo wamekuwa wakisita kukubali zoezi la kunyang’anywa silaha. Nchini Ivory Coast tayari wapo wanajeshi 6,000 wa umoja wa mataifa na wengine 4,000 kutoka Ufaransa nchi ambayo iliitawala Ivory Coast wakati wa ukoloni.