1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Vifaa vya silaha vimetoweka

6 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZI

Kuna ushahidi kuwa vifaa vya silaha vimeporwa nchini Iraq,tangu nchi hiyo kuvamiwa chini ya uongozi wa Marekani.Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na tume ya Umoja wa Mataifa.Tume hiyo iliyopewa jukumu la kutafuta silaha za maangamizi nchini Iraq imesema,picha za sateliti zaonyesha kuwa katika maeneo 90 yasiolindwa nchini humo, vifaa vya kutengenezea silaha vimeporwa.Wakaguzi wa silaha wamesema uporaji huo umetokea miaka miwili iliyopita.Maafisa wana khofu kuwa vifaa hivyo huenda ikawa vimo katika mikono ya wafuasi wa itikadi kali.