1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Tume huru yapendekeza mageuzi ndani ya Umoja wa Mataifa.

7 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEdU

Ripoti huru inayotazamiwa kutolewa baadae leo,inaeleza kufanyike mageuzi makubwa katika Umoja wa Mataifa,iwapo chombo hicho kikuu cha maamuzi ya ulimwengu kitataka kuzuia vitendo vya rushwa kwa siku za usoni.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan pamoja na Baraza la Usalama,kwa pamoja wamekuwa wakishutumiwa vikali kutokana na kuhusika na mpango wa mafuta kwa chakula nchini Iraq.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa Umoja wa Mataifa ulikuwa na kiasi cha fedha zinazofikia dola bilioni 64 kwa ajili ya mpango huo na ukafanya makusudi kumuachia kiongozi wa zamani wa Iraq,Saddam Hussein kuzichezea atakavyo.

Tume hiyo huru inayoongozwa na Mkuu wa masuala ya hazina wa zamani wa Marekani Paul Vlocker,imeeleza imegundua vitendo kadhaa vya magendo na rushwa,katika uchunguzi wao.