1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Somalia yataka kuondolewa vikwazo vya silaha na Umoja wa Mataifa

18 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEa0

Somalia imeutaka umoja wa Mataifa kuindolea vikwazo vya silaha ikisema kuwa vikwazo hivyo vinazuia juhudi za kuunda vikosi vyake vya usalama.

Akizungumza mbele ya mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa rais Abdullahi Yusuf alisema vikwazo vya silaha vilivyowekewa nchi yake tokea mwaka 1992 vinazuia pia kupelekwa kwa wanajeshi wa kulinda amani ili kuilinda serikali yake mpya.

Mwezi wa July Umoja wa Mataifa ulikataa kuindoshea vikwazo hivyo Somalia ukisema utalifikiria tena suala hilo la marufuku baada ya kupokea ripoti ya nchi za Afrika mashariki zinazotaka kuwapeleka wanajeshi wake kulinda amani nchini humo.