1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Mkutano wa viongozi duniani wamaliza kwa kuidhinisha mageuzi ya wastani ya Umoja wa Mataifa

17 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEaE

Viongozi wa dunia wameidhinisha mageuzi ya wastani ya Umoja wa Mataifa katika mkutano wa kilele wa siku tatu kuadhimisha miaka sitini ya Umoja wa Mataifa ambayo imekuwa na hatua ndogo ya maendeleo katika kupambana na umaskini,Ugaidi,Kukuza usalama na kulinda haki za binadamu.

Viongozi wa nchi na serikali 150 wamehudhuria mkutano huo wa kilele kujadili mageuzi ya Umoja wa Mataifa nc njia za kuupiga vita Ugaidi na Umaskini.

Hata hivyo lakini waziri mkuu wa Canada Paul Martin amesema amevunjika moyo kwa kuwa mkutano huo wa kilele ulishindwa kulipa madaraka zaidi baraza lililopendekezwa la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Joschka Fischer amesema waraka wa Umoja wa Mataifa juu ya mageuzi hautoshi kwa kuwa umekosa kuonyesha njia za wazi za kutatua matatizo ya dunia.

Muda mfupi kabla ya kupitishwa kwa waraka huo waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Ali Rodrigues alizishutumu taratibu za mazungumzo na kuzitaja kuwa za kioja na kwamba zinaendeleza maslahi ya mataifa makubwa dhidi ya mataifa yanayoendelea