1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York.Mjadala kuhusu katibu mkuu mpya wa umoja wa mataifa waanza.

21 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAQ

Hadhara kuu ya umoja wa mataifa imeanza mjadala wa nani akabidhiwe wadhifa wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa.

Waziri wa zamani wa fedha wa Afghanistan ametuma maombi yake, yeye ni wa sabaa kuwania nafasi ya Kofi Annan atakae kamilisha muhula wa pili wa miaka mitano Disemba 31 ijayo.

Balozi wa zamani wa Ujerumani katika umoja wa mataifa Gunta Pleuger anaamini wadhifa huo safari hii atakabidhiwa mwanasiasa kutoka Asia.

Katika mahojiano na kituo cha matangazo cha Deutschland Funk Bwana Ploiga amemsifu katibu mkuu wa sasa Kofi Annan anaetokea Ghana akisema.

“Kofi Annan amewacha nyayo pana ambayo kuifikia haitokuwa rahisi. Kofi Annan alikuwa katibu mkuu katika kipindi tete kupita kiasi cha mpito cha umoja wa mataifa na nnaamini atakumbukwa daima kuwa katibu mkuu aliyestahiki na aliyeleta mageuzi makubwa kupita yeyote aliyemtangulia, ingawa mwenyewe anasikitika hakuweza kuleta mengi kama alivyokusudia”.