1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Israel yaomba radhi kwa mauaji ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa

26 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG3t

Balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa bwana Dan Gillerman ameeleza masikitiko juu ya kuuawa walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon.

Walinda amani hao waliuawa baada ya majeshi ya Israel kukishambulia kituo cha Umoja wa Mataifa

Lakini balozi Gillerman amepinga madai ya katibu Mkuu Kofi Annan kwamba majeshi ya nchi yake yalikishambulia kituo hicho kwa kudhamiria.