1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Annan apendekeza mageuzi katika Umoja wa Mataifa

21 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFUz

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ametoa muito wa kupanuliwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Badala ya wanachama 15 waliokuwemo katika Baraza la Usalama,idadi hiyo iongozwe kuwa wanachama 24.Hiyo ni sehemu ya ripoti inayoeleza mipango ya Katibu Mkuu Annan,anaetaka kufanya mageuzi makuu katika Umoja wa Mataifa.Hii leo Annan ataitoa ripoti yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.Ripoti hiyo vile vile inasema Baraza la Haki za Binadamu lichukuwe nafasi ya Halmashauri ya Haki za Binadamu ya hivi sasa.Wanachama wa baraza hilo jipya wachaguliwe na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.Ripoti ya Annan pia inatoa muito kwa Baraza la Usalama kutayarisha sheria zitakazoeleza lini matumizi ya nguvu za kijeshi yanaweza kuidhinishwa.