1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Wakimbizi wa Darfur wanahitaji kulindwa

10 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFYK

Umoja wa Mataifa umetoa muito kwa Umoja wa Afrika kuchukua hatua zaidi kuwalinda wakimbizi katika eneo la mgogoro Darfur nchini Sudan ambako utumizi wa nguvu ungali ukiendelea dhidi ya wakimbizi.Mratibu wa misaada ya kiutu ya Umoja wa Mataifa,Jan Egeland mjini New York amesema,vikosi vya Umoja wa Afrika vilivyopelekwa Darfur vinawalinda wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya kiutu,lakini wakaazi wa Darfur hawalindwi dhidi ya mashambulio ya wanamgambo wa Kiarabu.Mwanzoni mwa juma,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan alizungumza na Baraza la Usalama la Umoja huo juu ya suala la kuwa na vikosi vyake katika jimbo la magharibi la Sudan.Lakini uamuzi bado haujapitishwa.