1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Vikwazo vya silaha kuregezwa

14 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG7m

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuregeza vikwazo vya silaha vilivyowekwa mwaka 1992 dhidi ya Somalia.Uamuzi huo unafungua njia ya kuwepo uwezekano wa kupelekwa vikosi vya amani vya kimataifa nchini Somalia.Umoja wa Afrika unaunga mkono pendekezo la kupeleka vikosi vya amani nchini Somalia kuimarisha serikali ya mpito ya ushirikiano nchini humo na kutoa msaada kwa rais Abdullah Yusuf.Wapiganaji wa Muungano wa Mahakama za Kiislamu,waliudhibiti mji mkuu wa Somalia,Mogadishu mapema mwezi wa Juni na wakawatimua wababe wa vita wanaoungwa mkono na Marekani.Tangu serikali ya Siad Barre kupinduliwa miaka 15 ya nyuma,nchi hiyo kwenye Pembe ya Afrika imeshuhudia vurugu na mmuagiko mkubwa wa damu.