1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: UN yaombea misaada Wairani

30 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFno

Umoja wa Mataifa umetoa mwito wa dharura wa misaada zaidi ya kigeni kwa ajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi ambalo limeuwa kiasi ya watu elfu 30 kusini mashariki mwa Iran. Mashirika ya kimataifa yametoa kiasi cha Dola nusu milioni kama mchango wake katika mfuko huo maalum wa msaada wa dharura kwa ajili ya wakaazi wa mji wa Bam uliotikiswa vibaya na tetemeko hilo ijumaa iliopita. Pamoja na tafauti za kisiasa kati yake na Iran, serikali ya Marekani imetuma ndege ya misaada ya dharura, yakiwemo madawa na kuahidi misaada zaidi siku zijazo. Nchi za kiarabu za ghuba zimekubali pia kutenga kiasi ya Dola Milioni 400 kusaidia watu zaidi ya laki moja walionusurika katika janga hilo. Wakati huo huo, polisi na askari wa Iran wametumwa eneo hilo baada ya waporaji kushambulia misafara ya magari ya misaada ya dharura.