NEW YORK: UN kuafikiana na US juu ya Iraq
20 Januari 2004Matangazo
Umoja wa Mataifa umeanza kutafakari pendekezo la Marekani na serikali ya mpito ya Iraq ya kumuomba Katibu Mkuu Kofi ANNAN atume wajumbe wake kwenda Baghdad kuangalia iwapo mazingira yaliopo yanatoa fursa ya kufanyika uchaguzi kabla ya mwisho wa mwaka huu. Matokeo ya ziara hiyo yanatarajiwa kusaidia kuondoa tafauti kati ya Marekani na kiongozi mkuu wa Washi'a wa Iraq kuhusu masharti ya Marekani kuwakabidhi Wairaki madaraka ifikapo Juni 30 kama ilivyotakiwa na Umoja wa Mataifa.