1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Umoja wa Ulaya wataka Iran ifikishwe mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa

18 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZt

Umoja wa Ulaya unataka Iran ifikishwe mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa mpango wake wa nyuklia. Uwezekano wa Iran kufikishwa mbele ya baraza hilo uliongezeka wakati rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad alipohutubia katika mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa mjini New York, Marekani.

Kiongozi huyo alisisitiza kwamba nchi yake ina haki ya kuendelea mbele na mpango wake wa nyuklia na kwamba Marekani haina haki yoyote ya kuuzuia mpango huo wa Iran, kwani Marekani ndilo taifa pekee ambalo limewahi kutumia silaha za nyuklia.

Msemaji wa umoja wa Ulaya ameelezea wasiwasi wake kuwa sasa jumuiya ya Ulaya haina chaguo lengine ila kuishitaki Iran kwa baraza la usalama la umoa wa mataifa ili iwekewe vikwazo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Philippe Douste-Blazy amesema swala hilo bado linaweza kujadiliwa.