1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Umoja wa Mataifa walilaani shambulio la Israel dhidi ya mji wa Qana

30 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG2P

Umoja wa Mataifa umelilaani shambulio la Israel katika mjiw a Qana lililowaua watu 54, wakiwemo watoto 37. Umoja huo umetoa mwito mapigano yasitishwe.

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Geir Pedersen, amesema ameshutushwa na kuhuzunishwa na mauaji ya walebanon na ametaka shambulio hilo lichunguzwe.

Viongozi mbalimbali ulimwenguni wameikosoa pia Israel kwa shambulio la Qana. Rais wa Ufaransa, Jacques Chirac amesema Ufaransa inakilaani kitendo cha Israel akisema hakiwezi kukubalika.

Mfalme Abdullah wa Jordan, kiongozi wa kwanza wa taifa la kiarabu kuzungumzia vita va Lebanon, amesema ni kitendo cha unyama na ni uvunjaji wa sheria za kimataifa.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert, amelitetea shambulio la mjini Qana akisema eneo hilo linatumiwa na kundi la Hezbollah kuvurumishia maroketi kuelekea Israel na kwamba raia walionywa waondoke.

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, amesema shambulio hilo ni uhalifu na kuutaka Umoja wa Mataifa uingilie kati kuumalza mgogoro huo.

Mkutano wa dharura wa mataifa ya kiiislamu utafanyika mjini Kuala Lumpur nchini Malaysia Alhamisi ijayo kujadili vita vya Lebanon. Mataifa yatakayohudhuria ni Saudi Arabia, Qatar, Senegal, Yemen, Uturuki, Azerbaijan na Malaysia.