1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York-Umoja wa Mataifa waleza hali mbaya ya mateso mashariki mwa Kongo.

17 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWH

Umoja wa Mataia umesema kuwa wanamgambo katika eneo la Mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamekuwa wakiendesha vitendo vya utekaji nyara,mateso na mauaji kwa mamia ya raia wanaotoka katika makundi ya kikabila yanayohasimiana.Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeorodhesha maovu yanayofanywa katika eneo la kaskazini-mashariki linalopakana na Uganda,katika ripoti yake baada ya kukusanya ushahidi kutoka kwa watu walionusurika kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya dharura,Jan Egeland amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la Mashari mwa Congo limekumbwa na madhila makubwa ya kibinadamu ambayo hayajawahi kuonekana katika miaka ya hivi karibuni duniani.Ameongeza kuwa ni jambo la kushangaza kuona dunia ilikaa kimya kutokana na mateso waliyokuwa wanayapata watu wa eneo hilo.