1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK-Umoja wa Mataifa waidhinisha vikosi vyake vya kulinda amani kuendelea kubakia Congo kwa miezi sita zadi.

31 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFRi

Umoja wa Mataifa umepiga kura kuafiki vikosi vyake vya kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo viendelee kubakia huko kwa miezi sita mingine.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,halikadhalika limetoa baraka kwa wanajeshi 17,000 wa kulinda amani kutumia uwezo wao kuwalinda raia,watakaokabiliwa na vitisho kutoka kikundi chochote cha wanamgambo wenye silaha.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinasaidia kazi ya utekelezwaji wa mkataba wa amani wa mwaka 2003,ambao ulimaliza miaka mitano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.