1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Umoja wa Mataifa kupata askari 3500 karibuni

16 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDLC

Umoja wa Mataifa umesema, unatumai kupata askari alfu 3500 mnamo muda wa wiki mbili ,ikiwa ni sehemu ya jeshi la kulinda amani kusini mwa Lebanon.

Askari hao watasaidia kuimarisha hatua ya kumaliza mapigano na kusimamia zoezi la kuyawezesha majeshi ya Lebanon kuingia kusini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya Lebanon, askari alfu 15 watahitajika katika kutekeleza jukumu la kulinda amani nchini humo. Lakini hadi sasa haijafahamika ni nchi gani zitakazochangia askari wa jeshi hilo.