1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK. Tume ya amani ya umoja wa mataifa itaendelea kubakia Ivory Coast.

5 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQ6

Baraza la usalama la umoja wa mataifa, limepiga kura hii leo kurefusha muda wa tume ya kulinda amani nchini Ivory Coast, kwa mwezi mmoja. Wanajeshi elfu sita wa umoja huo na wanajeshi elfu nne wa Ufaransa, wanalinda amani katika eneo lililokumbwa na machafuko nchini humo. Mamlaka ya tume hiyo ilimalizika rasmi hapo jana. Baraza hilo pia lilitoa wito mpya kwa waasi na wanajeshi wa serikali kujitolea kwa dhati katika juhudi za kuleta amani. Wakati huo huo, rais Thabo Mbeko wa Afrika Kusini, anaendelea na mazungumzo na viongozi wa Ivory Coast kuumaliza mzozo huo wa miaka mitatu.