1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Syria haitaki kushirikiana na uchunguzi wa umoja wa mataifa.

26 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEhe

Syria inashindwa kushirikiana na uchunguzi wa umoja wa mataifa unaoongozwa na mwendesha mashtaka kutoka Ujerumani Detlev Mehlis kuhusiana na kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri , Februari mwaka huu.

Afisa mwandamizi wa umoja wa mataifa ameliambia baraza la usalama katika kikao cha faragha .

Ibrahim Gambari , msaidizi wa katibu mkuu, akihusika na masuala ya kisiasa, amesema kuwa Syria imeshindwa kutoa majibu ya maombi ya nyaraka na mahojiano kwa muda wa wiki sita sasa.

Mehlis anatarajiwa kukutana na maafisa wa Syria leo Ijumaa, lakini balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa John Bolton, amesema hiyo haitoshi.

Balozi wa Syria katika umoja wa mataifa Fayssal Mekdad, amesema kuwa nchi yake ina nia ya kushirikiana katika uchunguzi huo.

Wengi wanaamini kuwa Syria inahusika katika kifo cha waziri mkuu Rafik Hariri. Syria inakana kuhusika kwa aina yoyote katika mauaji hayo.