1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Silaha bado zinanunuliwa Somalia.

15 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWt

Silaha bado zinamiminika nchini Somalia katika kiwango cha kutisha , licha ya kupingwa marufuku na umoja wa mataifa mwaka 1992, na kuhatarisha juhudi za kurejesha madarakani serikali mpya.

Wachunguzi wa umoja wa mataifa wamesema jana kuwa licha ya kupanda kwa bei, watu binafsi kutoka katika serikali mpya ya mpito na makundi ya upinzani wananunua silaha katika soko la magendo.

Kwa mujibu wa ripoti ya kundi linalochunguza mwenendo wa silaha katika eneo hilo, imependekezwa kuweka ulinzi mkali katika mipaka ya pwani ya Somalia.