1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Mkutano wa UN waanza leo.

14 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEbH

Baraza kuu la umoja wa mataifa limeidhinisha muswada wa mpango wa mageuzi kwa ajili ya taasisi hiyo ya kimataifa katika mkesha wa mkutano wa viongozi wa dunia mjini New York.

Viongozi 170 wanatarajiwa kuidhinisha waraka huo, ambao wakosoaji wanasema kuwa ni waraka uliopunguzwa sana makali kutoka vile katibu mkuu wa umoja huo Kofi Annan alivyotarajia.

Hata hivyo Annan amewaambia waandishi wa habari kuwa hatua za mageuzi zitaendelea.

Muswada huo unalenga katika masuala kadha , ikiwa ni pamoja na maendeleo, haki za binadamu, ugaidi na usalama duniani.

Mkutano huo wa siku tatu, unaoanza leo Jumatano, umeelezwa kuwa utawahusisha viongozi wengi zaidi , katika historia ya umoja huo.