1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Mkutano wa Kilele wa wamalizika kwa mageuzi ya wastani kwa Umoja wa Mataifa

17 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEaO

Viongozi wa dunia wameidhinisha mageuzi ya wastani ya Umoja wa Mataifa hapo jana baada ya mkutano wa kilele wa siku tatu kuadhimisha miaka 60 ya Umoja wa Mataifa ambayo yamekuwa na hatua ndogo ya maendeleo katika kupiga vita umaskini na ugaidi,kukuza usalama na kulinda haki za binaadamu.

Wakuu wa nchi na serikali 150 wamehudhuria mkutano huo wa kilele kujadili mageuzi ya Umoja wa Mataifa na njia za kupiga vita ugaidi na umaskini.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameyakaribisha makubaliano juu ya kuwajibika kimataifa katika kuingilia kati ili kulinda raia kutokana na mauaji ya halaiki na utokomezaji wa kizazi fulani hiyo kuzuwiya marudio ya mauaji ya Rwanda,Bosnia na Kosovo.

Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Yoschka Fischer amesema kwenye hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba azimio hilo halitoshi.

Mataifa mengi yanayoendelea pia yamelishutumu azimio hilo kwa kusema kwamba limeonyesha kupigwa kwa hatua chache za maendeleo juu ya masuala kama vile kupiga vita umaskini na kulinda haki za binaadamu.

Muda mfupi kabla ya kupitishwa kwa azimio hilo lenye kurasa 40 waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Ali Rodrigues ameshutumu taratibu za mazunguzo kuwa za kioja na kusema kwamba zinaendeleza maslahi ya mataifa kubwa dhidi ya mataifa yanayoendelea.