1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mataifa ya G4 na umoja wa Afrika yashindwa kukubalina juu ya kupanuliwa kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa

18 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtO

Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka Ujerumani, Brazil, India na Japan, wameshindwa kufikia makubaliano na umoja wa Afrika juu ya mapendekezo yao ya kutaka baraza la usalama la umoja wa mataifa lipanuliwe. Hata hivyo wamekubaliana kuendelea na mazungumzo zaidi mjini Geneva baada ya wiki moja.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer, amewaambia waandishi habari mjini New York, Marekani, kwamba hakutakuwa na mabadiliko kuhusiana na haki ya kuwa na kura ya turufu kwa wanachama wapya wa baraza hilo.

Pendekezo lililotolewa na mataifa ya G4 linataka wanachama wapya wasiwe na kura ya turufu. Lakini kwa upande mwingine pendekezo lililowasilishwa na umoja wa Afrika linataka wanachama wapya wawe na haki ya kura ya turufu.