1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mapigano nchini Congo yaongeza wakimbizi

19 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFVV

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,watu kwa maelfu wamehamia kambi za wakimbizi au wamekimbilia porini kwa sababu ya mapigano yaliozidi katika sehemu za Ituri kaskazini- mashariki mwa nchi.Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa Umoja wa Mataifa Fred Eckhard,zaidi ya watu 88,000 wanapokea misaada ya kiutu katika eneo la Djugu huko Ituri,baada ya kuyakimbia mapigano yaliozuka mwishoni mwa mwaka jana.Wasaidizi wa Umoja wa Mataifa wana khofu zaidi kuhusu wale wanaokosa kupata misaada kwa sababu wamekimbilia porini na ni shida kufika katika maeneo hayo.Ituri ni jimbo lenye utajiri wa dhahabu,almasi na mbao lakini limevurugwa kwa mapigano ya kikabila na ya makundi yanayohasimiana.