1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mapendekezo ya kufanywa mageuzi katika Umoja wa Mataifa

4 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7A

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,Jean Ping ametoa mswada wa mapendekezo ya kufanywa mageuzi kadhaa katika Umoja huo.Mswada uliotayarishwa kuambatana na majadiliano yaliofanywa kati ya madola 191 ya Umoja wa Mataifa mjini New York,unashauri kuwa Halmashauri ya Umoja wa Mataifa,inayoshughulikia haki za binadamu ivunjwe.Imependekezwa kuwa Baraza Kuu lichague Kamisheni mpya itakyochukua nafasi ya halmashauri iliyopoteza sifa.Kwa wakati huo huo Ping ambae ni rais wa Gabon,ametoa wito kwa wanachama wa Umoja wa Mataifa kuimarisha zaidi juhudi za kutetea haki za binadamu na kupambana na umasikini.