1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Kura ya mswada imeahirishwa Umoja wa Mataifa

8 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG9e

Japan katika Umoja wa Mataifa imependekeza rasmi mswada wa azimio litakaloiwekea vikwazo Korea ya Kaskazini.Lakini kura kuhusu azimio hilo haitopigwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kabla ya Jumatatu.Japan ilipendekeza kuwa mswada huo upigiwe kura siku ya Jumamosi.Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa,Wang Guangya alionya kuwa pindi mswada huo utapigiwa kura,basi”hakutokuwepo umoja” katika baraza la usalama.Mswadaa wa azimio hilo umependekezwa baada ya Korea ya Kaskazini kufanya si chini ya majeribio saba ya makombora,siku ya Jumatano.Miongoni mwa makombora hayo,moja ni la masafa marefu.Kwa maoni ya baadhi ya wataalamu, kombora hilo lina uwezo wa kufika hadi Alaska nchini Marekani.Maafisa wa Kimarekani wamesema, kombora hilo liliruka kwa muda uliopungua dakika moja na liliangukia baharini magharibi ya Japan.