1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Kofi Annan kupokea ripoti ya uchunguzi wa kifo cha Hariri

20 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEQ5

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan, ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa kuisadia Pakistan ili kuzuia kuongezeka kwa idadi ya vifo vilivyosababishwa na tetemeko la ardhi nchini humo. Annan amesema watu takriban milioni tatu wameachwa bila makao wakiwa hawana mablanketi wala mahema ya kujikinga.

Wakati huo huo, India na Pakistan zimekubaliana kuwasaidia waathiriwa wa tetemeko hilo kwa kuwaruhusu kuvuka eneo linalozitengenesha nchi hizo. Waziri wa habari nchini Pakistan, Sheikh Rashid, amesema atapeleka malori 25 ya misaada inayohitajika kwa dharura na waathiriwa katika eneo linalomilikiwa na India la Kashmiri. Ameyasema hayo siku mbili baada ya rais wa Pakistan, Pervez Musharaf, kutaka raia wa Kashmiri waruhusiwe kuvuka eneo lililo chini ya ulinzi mkali, ili kuwasaidia waathiriwa wa janga hilo.

India iliyashuku mapendekezo kama hayo kabla tetemeko kutokea ikiilaumu Pakistan kwa kuwadhamini wapiganaji katika upande wake wa Kashmir.