1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Kofi Annan ataka jumiya ya kimataifa kuisaidia Pakistan.

20 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEQ9

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Pakistan kuweza kuzuwia wimbi la pili kubwa la vifo kutokana na tetemeko kubwa la hivi karibuni.

Annan amewaambia waandishi wa habari kuwa kiasi cha watu milioni tatu hawana mahali pa kuishi, wakiwa hawana mablanketi ama mahema kuweza kuwazuwia na baridi kali.

Pakistan na India wamekubaliana hivi karibuni kuwasaidia wahanga wa tetemeko hilo la ardhi katika jimbo la Kashmir kwa kuruhusu watu kutembeleana kupitia mpaka unaotenganisha jimbo hilo linalogombaniwa.

Rais wa Pakistan Pervez Musharaff , amesema kuwa hatua hiyo ina lengo la kuwasaidia mamia kwa maelfu ya watu walionusurika kutokana na tetemeko hilo siku 10 zilizopita ambao bado wanahitaji sana msaada.

Wakati huo huo , idadi mpya iliyotolewa na maafisa wa kimkoa nchini Pakistan inaonyesha kuwa watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo inafikia sasa watu 48,000.