1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Kofi Annan aahirisha mabadiliko ya baraza la usalama la umoja wa mataifa

11 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CElu

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan ameyaahirisha mabadiliko ya baraza la usalama la umoja huo hadi mwezi Disemba mwaka huu.

Hapo awali alitaka mabadiliko hayo yakamilike kufikia mwezi Septemba, wakati viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanapotarajiwa kuidhinisha mapendekezo ya mageuzi ya baraza hilo katika mkutano wa kilele kabla kufanyika mkutano wa kila mwaka wa baraza kuu la umoja wa mataifa.

Lakini mataifa wanachama bado yanajaribu kupunguza tofauti zilizopo juu ya mapendekezo ya mabadiliko muhimu, yakiwemo kupanuliwa kwa baraza hilo la usalama, maana halisi ya ugaidi, bajeti na mageuzi ya maongozi.