1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameitaka...

9 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFtt
Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia Afghanistan ili kuepusha na uwezekano wa kutofanikiwa na utaratibu kuijenga demokrasia, na ikakumbwa na vitendo vya kigaidi. Mashambulio ya kigaidi, biashara ya madawa ya kulevya na mapigano ya makabila, yanahatarisha uchaguzi uliopangwa kuitishwa mwaka ujao, - kwa mujibu wa ripoti ya Annan ikihusika na Afghanistan. Wakati huo huo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anaandaa kuitisha mkutano wa kimataifa kuzungumzia hali ya Afghanistan. Mkutano huo unatakiwa kuimarisha msaada wa kiuchumi na kisiasa ambao ulikubaliwa kwenye mkutano wa Petersburg, mjini Bonn, kuusaidia utataribu wa mpito katika nchi hiyo.