1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashutumiwa katika ripoti iliyochunguza kashfa ya mpango wa chakula kwa mafuta nchini Iraq.

30 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFSC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan,ameshutumiwa katika ripoti inayohusu Umoja wa Mataifa na mpango wake wa mafuta kwa chakula nchini Iraq.Ripoti hiyo ya mpito hata hivyo imemsafisha Bwana Annan kwa kutofanya jambo lolote lililokwenda kinyume,lakini imesema uchunguzi Bwana Annan alioufanya kuhusiana na kujihusisha kwa mwanawekatika kashfa hiyo ulikuwa na upungufu.

Alipoulizwa iwapo atajiuzulu wadhifa wake wa Ukatibu Mkuu,Bwana Annan alisema hata iweje haiwezekani.

Mwaka 1998 kampuni moja ya Uswiss iliyomuajiri mwanawe Annan,Kodjo Annan,ilipewa mkataba na Umoja wa Mataifa kuhakiki bidhaa zilizokuwa zinaigizwa Iraq.Kodjo Annan wakati huo alikuwa akifunzwa kazi na kampuni ya Cotecna.

Ripoti hiyo imehitimisha kwa kueleza kuwa Bwana Annan hakutumia uwezo wake kufanikisha kampuni ya Cotecna kupatiwa mkataba huo.Halikadhalika ripoti hiyo imeeleza kuwa Kodjo Annan,kwa makusudi alimdanganya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya yeye kuendelea na uhusiano wake kifedha na kampuni hiyo.