1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK :Gambari awa kiongozi wa idara ya siasa ya Umoja wa Mataifa

11 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF4w

Ibrahim Gambari wa Nigeria balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa,profesa na aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje hapo jana amechaguliwa kuwa mkuu wa idara ya siasa ya Umoja wa Mataifa yenye hadhi kubwa.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Gambari mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Afrika tokea mwaka 1999 atatumikia wadhifa huo hadi mwishoni mwa mwaka 2006 wakati muhula wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan unapomalizika na anachukuwa nafasi ya Kieran Prendergast wa Uingereza ambaye anajiuzulu mwezi huu.

Idara hiyo ya masuala ya kisiasa yenye wafanyakazi 240 inafuatilia migogoro duniani kote,inapendekeza sera kwa katibu mkuu na Baraza la Usalama pamoja na kutowa msaada wa uchaguzi na kusuluhisha mizozo.