1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK. Chakula kwa wakimbizi Afrika kupunguzwa?

20 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFC6

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema ,huenda likalazimika kupunguza migao ya chakula kwa wakimbizi barani Afrika ikiwa kama wafadhili hawatatimiza ahadi zao.

Shirika hilo linalotenga robo tatu ya bajeti yake kwa ajili ya bara la Afrika linakabiliwa na upungufu wa dola milioni 315.Nchi ambazo tayari zimeshaathirika na upungufu huo ni Sierra Leone,Guinea na Liberia.

Pia limesema kwamba akiba ya chakula kwa ajili ya wakimbizi wa Sudan waliopo nchini Uganda imepungua.

.