1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Baraza la usalama la umoja wa mataifa lashutumu mauaji Iraq.

9 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEw1

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeshutumu mauaji ya mjumbe wa ngazi ya juu wa ubalozi wa Misr nchini Iraq, Ihab el- Sharif.

Katika taarifa ya pamoja , baraza hilo limeshutumu mashambulizi yote dhidi ya wafanyakazi raia wa kigeni nchini Iraq.

Tawi la mtandao wa kigaidi wa al Qaeda nchini Iraq limesema kuwa limemuua el-Sharif baada ya kumteka nyara mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wakati huo huo Misr imesema kuwa itapunguza wafanyakazi wake katika ubalozi huo mjini Baghdad kufuatia kifo cha el-Sharif.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Misr Ahmed Aboul Gheit amesema kuwa upunguzaji huo ni juhudi za kuwalinda wafanyakazi katika ubalozi huo.

Lakini wizara ya mambo ya kigeni ya Iraq imezitaka nchi za Kiislamu na zile za Kiarabu kutoyumbishwa na ghasia za wapiganaji wa chini kwa chini.