1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lashindwa kukubaliana

27 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG3e

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kukubaliana juu ya maneneo ya azimio la mauaji ya wanajeshi wanne wa kulinda amani yaliyofanywa na Israel kusini mwa Lebanon.

Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Jean Marc de Sabliere, amesema Marekani ililitilia guu azimio hilo ambalo lingeikosoa Israel kwa shambulio lake.

Hapo awali katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, alieleza kuvunjwa moyo na hatua ya Israel kupuuza miito ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wakitaka mashambulio dhidi ya kituo chao yakomeshwe.

Wakati haya yakiarifiwa, Australia imetangaza itawaondoa wanajeshi wake katika Umoja wa Mataifa kutoka kusini mwa Lebanon. Waziri wa ulinzi Brendan Nelson amewaambia waandhishi habari mjini Canberra kwamba wanajeshi hao watahamishwa kwenda mjini Beirut.