1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ban Ki Moon amkosoa rais Bush kwa kuiwekea vikwazo Sudan

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwb

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amemkosoa vikali rais wa Marekani, George W Bush, kwa uamuzi wake wa kuiwekea vikwazo vipya dhidi ya serikali ya Sudan.

Hapo jana rais Bush alitangaza ataongeza vikwazo dhidi ya Sudan kuibinya ikomeshe umwagaji damu unaoendelea katika jimbo linalokabiliwa na mzozo la Darfur.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema anawasiliana na serikali ya Sudan na anaamini muda zaidi unahitajika kuishawishi serikali ya mjini Khartoum ikubali kikosi cha kulinda amani Darfur kitakachowajumulisha wanajeshi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

´Kuhusu vikwazo na diplomasia nadhani kunaweza kuwa na ushirikiano. Ipo haja, ikizingatiwa jinsi serikali ya Sudan ilivyokuwa ikiushughulikia mzozo wa Darfur, kuendelea kuibinya.´

China, Misri na jumuiya ya nchi za kiarabu pia zimeikosaoa Marekani kwa kuiwekea vikwazo Sudan. Sambamba na hayo, serikali ya Ujerumani imetangaza kwamba inapanga kuwapeleka wanajeshi 200 kwenda Darfur katika wiki chache zijazo.