1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK-Antonio Guterres achaguliwa mkuu mpya wa UNHCR.

25 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAa

Umoja wa Mataifa umemteua Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno,Antonio Guterres kuwa mkuu mpya wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi-UNHCR.Bwana Guterres anachukua nafasi ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uholanzi,Ruud Lubbers,ambaye alishinikizwa kujiuzulu mwezi wa Februari mwaka huu,kufuatia tuhuma za kumdhalilisha mwanamke mmoja kijinsia ambazo hata hivyo alizikanusha vikali.

Bwana Guterres katika nafasi hiyo mpya ya ukuu wa UNHCR,aliwapiga kumbo wagombea wengine saba waliokuwa wakiwania nafasi hiyo,akiwemo Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Australia,Gareth Evans.

Bwana Guterres aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Ureno kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2001.