1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Annan ana imani na mageuzi ya Umoja wa Mataifa

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF72

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ametowa wito mpya kwa viongozi wa serikali kusaidia kuufanyia mabadiliko Umoja wa Mataifa.

Amesema kwamba chombo hicho cha dunia hakina budi kuchukua hatua muhimu kupunguza kiwango cha umaskini kwa nusu duniani ifikapo mwaka 2015 na kupiga vita ugaidi wa kimataifa.

Pia amesema ana imani kwamba Umoja wa Mataifa utaridhia agenda yake ya mageuzi makubwa katika mkutano wake wa viongozi mwezi wa Septemba mjini New York.