1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New-York: Aliyekua mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini ...

16 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFin
Afghanistan,LAKHDAR BRAHIMI ameteuliwa kua mshauri mkuu wa jumuia hiyo ya kimataifa.Katibu mkuu Kofi Annan amemteuwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 kuwa mshauri wake mkuu katika masuala ya amani na usalama.Kwa namna hiyo bwana LAKHDAR BRAHIMI anashughulikia pia suala la Iraq.Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nchi za nje wa Algeria anajivunia sifa kubwa miongoni mwa wanadiplomasia wa Umoja wa mataifa.