1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK Afrika yawasilisha azimio lake kwa baraza kuu la umoja wa mataifa

14 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEug

Azimio la Afrika linalotaka kuundwe viti sita vipya katika baraza la usalama la umoja wa mataifa vitakavyokuwa na kura ya turufu, limewasilishwa mbele ya baraza kuu la umoja wa mataifa. Azimio hilo lakini halikuwasilishwa na muungano wa mataifa ya Afrika , ila na baadhi ya mataifa hayo kwa niaba ya yale mengine.

Afrika inataka baraza la usalama lipanuliwe na kuwa na wanachama 26 na ipate viti viwili vya kudumu na vingine viwili ambavyo havitakuwa vya kudumu katika baraza hilo.